BAADHI ya
wakulima wa mboga na matunda wilayani Lushoto wanaiomba serikali nawadau wa
maendeleo kuwakopesha vitendeakazi ikiwemo gari la kutunza ubaridi (coldcars)
ili waweze kusafirisha mazao yao yakiwa katika ubora wa kijani unaohitajika sokoni.
Wametoa ombi hilo kwa nyakati tofauti katika
mahojiano na mwandishi wetu wa sauti
yetu wanatanga kuhusu utekelezaji wa
Mpango wa Uzalishaji wa Mazao ya Mboga na Matunda kulingana na mahitaji ya
Soko.Mpango huo ambao niwa majaribio katika vikundi viwili vya wakulima wilayani Lushoto umepewa kaulimbiu isemayo 'Anza na utafiti wa Masoko kwanza ', unatekelezwa kwa ushirikiano wa ufadhili baina ya serikali ya Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Maendeleo (JICA).
Mmoja wa wakulima hao aitwae Gasper Emmanuel kutoka kikundi cha wakulima cha Besha alisema utekelezaji wa hatua hiyo utawawezesha kujihakikishia soko lililopo kwa kuhimili ushindani na hivyo kuimarisha uzalishaji wa mazao hayo na kupato zaidi.
"Mpango huu wa kufanya utafiti wa soko kabla ya kutayarisha zao umetupunguzia hasara kwasababu sasa mkulima anatayarisha zao kulingana na uhitaji na ubora anaotaka mnunuzi.
Pia imetuongezea
kuaminiwa sokoni kwahivyo naomba serikali itukopeshe cold cars ili tuweze
kusafirisha mazao yetu yakiwa katika hali ya kijani ,"alisema Emmanuel.
Awali Afisa Kilimo wilaya ya Lushoto, Hasani Shelukindo akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Mwakilishi Mkuu wa Jica Tanzania, Tashio Magase na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigila alisema mradi huu umeleta mafanikio makubwa kwa wakulima.
"Utafiti wetu umeonyesha kwamba kipato cha mkulima katika vijiji vya majaribio umeongezeka kwa asilimia 78 na pato la kaya kwa ujumla limeongezeka kwa asilimia 54 ikilinganishwa na mwanzoni ambapo walilazimika kuuza mazao kwa bei ndogo zaidi isiyolingana na gharama za uzalishaji," .
Alisema takwimu za utafiti huo zimekusanywa kuanzia mwaka 2013 hadi mwishoni mwa mwaka jana katika vijiji vya Maringo, Kwesime na Boheloi ambako mpango huo unatekelezwa kwa majaribio.
Kwa upande wake Toshio Magase aliwapongeza wakulima na kuwataka waendelee kuhamasisha wengine wengi zaidi ili waweze kupokea teknolojia mpya za uzalishaji mazao ikiwemo kutumia matuta, mbolea pamoja na kufuata jedwali la mahitaji makubwa ya soko.
Uzalishaji wa Mboga na Matunda katika halmashauri ya wilaya ya Lushoto unakadiriwa kufikia tani 189,974 kwa mwaka kutegemeana na msimu, wadudu na magonjwa ambapo asilimia 10 kati ya hizo hutumika nyumbani, asilimia 60 huuzwa kwenye masoko yaliyopo nje ya wilaya na asilimia 20 huharibika kwa kukosa wanunuzi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni