Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martin Shegela amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya zote
za mkoa wa Tanga kuanza mara moja kutumia mshine za kilelektroniki katika
ukusanyaji wa mapato na ili kuthibiti udanganyifu katika Hamashauri zao.
Akizungumza katika kikao kazi na wakuu wa
wilaya, wakurugenzi, na wakuu wa idara zote za mkoa wa Tanga kilichofanyika leo
kwenye ukumbi wa Halmasauri ya jiji la Tanga kwa kwa lengo la kutambua
changamoto zilizopo katika kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato, Mkuu wa mkoa
amasema ni lazima kujituma na kufikia malengo kwa kuhakikisha matumizi sahihi ya
mashine za kilelektroniki, kama linavyoekelea agizo lililo tolewa na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Amesema Wakuu wote wa idara mkoani hapa
wanapaswa kulenga ukusanyaji wa mapato wa kiwango cha juu, kwa Halmashauri kutumia
mashine hizo za kielektroniki kwani kwa kutumia mashine hizo wataweza kuepuka upotevu,
kwa kila kinachokusanywa na anayekusanya kuoneshwa kupitia mashine hizo.
Naye mkurugenzi wa jiji la Tanga Bw Daudi
Mayeje ametoa maelekezo ya namna ya kutumia mshine ambazo idara za jiji la
Tanga zimeanza kuzitumia na kusema kuwa mfumo huo unaonesha mafanikia makubwa ya
ukusanyaji wa mapato.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni