Jumamosi, 23 Julai 2016

MIGOGORO YA ARDHI INAENDELEA KUTIKISA WILAYA YA KILINDI MKOANI TANGA.



Wananchi wa wilaya ya Kilindi wameiomba serikali kuharakisha inamaliza tatizo la mpaka kati yake na wilaya ya Kiteto ili kumaliza mapigano kati ya wakulima na Wafugaji.

Maombi hayo wameyatoa mbele ya Naibu Waziri wa Nyumba na maendeleo ya Makazi Angelina Mabula Wakati wa ufunguzi wa baraza la ardhi katika wilaya ya Kilindi.

Walisema tatizo la mpaka limedumu Kwa zaidi ya miaka 20 bila ya kupatiwa ufumbuzi wa aina yoyote huku wananchi wakiendelea kujeruhiwa na Hata wengine kuuwa kwa mapigano.

 Mmoja wa wananchi hao Ali Mbwego alisema Mara Kwa Mara wataalamu wa ardhi wamekuwa wakija katika wilaya hiyo Kwa ajili ya kutafuta mipaka lakini mpaka sasa hakuna mafanikio yoyote.

"Kuna hitajika viongozi waadilifu katika kushughulikia mgogoro wa mipaka kwani licha ya kuwepo Kwa ramani lakini bado rushwa imetawala katika kumaliza tatizo hilo, hivyo tunaimani Rais  Magufuli atamaliza mgogoro huo" alisema Mbwego.

Naye Hassan Masoli mkazi Kilindi alisema mpaka wa Kiteto umekuwa kila siku ukiongezeka na kuingia wilaya ya Kilindi Kwa ajili ya kuwalinda Wafugaji na kuwaacha wakulima wakiwa hawana maeneo ya kulima.

 Pia Naibu Waziri Mabula amewataka wananchi na wakazi wa kilindi kuwa watulivu  alisema kuwepo Kwa baraza la ardhi katika Wilaya hiyo ni hatua moja wapo ya kushughulikia kero za ardhi zilidumu Kwa muda mrefu.

 “Ujio wa baraza ulitokana na uhitaji mkubwa kutoka na wilaya hiyo kuwa na zaidi ya kesi 204 pekee ambazo zilikuwa zinasikilizwa wilaya ni Korogwe”. alisema Naibu Waziri Mabula


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni