Jumatano, 27 Julai 2016

DAMPO LA KATA YA MZINGANI MKOANI TANGA LAWAKERO KWA WANANCHI.





 
Wakazi wa kata ya Mzingani wameiomba  Halmashaul ya Jiji la Tanga kuwaondolea taka kwa wakati katika Dampo lililopo jirani na makazi yao kwani linaweza kuwasababishia magonjwa ya mlipuko.

Akizungumzia kero hiyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Mzingani Muhamed Kalua alisema Dampo hilo ambalo liko jirani na Makaburi halithaminiwi na viongozi wa Jiji hilo na halizolewi takataka kwa wakati kiasi kwamba linawatesa wananchi wa Mtaa huo.

Naye Mwenyekiti wa mtaa Kalua alifika Halmshauri na kuzungumza na viongozi nao walimwahidi kulifanyia kazi Dampo hilo ndani ya siku kadhaa na mpaka sasa hakuna kilichofanyika.

Wakazi wa Mtaa wa Mzingani  wanaokaa jirani na Dampo hilo  wameomba viongozi wa Jiji kulihamisha Dampo hilo kwani liko jirani makazi yao pia linachafua  ya eneo la makaburi tulipozikia ndugu zetu.
 
Pia Sauti yetu wanatanga ilifanya jitihada za kutafuta kiongozi wa Jiji  ilikuweza kupata ufafanuzi wa swala hilo na kumpata Meya wa Jiji Tanga Mustafa Mhina ambaye alisema ipo changamoto kubwa ya Madampo katika Jiji la Tanga na mpaka sasa tunajitahidi kukabiliana nalo ili kuhakikisha taka zilizopo kwenye Madampo zinazolewa.

Meya wa Jiji la Tanga Mustafa Mhina amewataka wananchi na wakazi wa kata ya Mzingani kuwa wavumilivu kwani kwasasa Halmashaul  ya Jiji imeshapokea vifaa vya usafi mara kibali kitakapo tolewa vitaanza kazi.    

 





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni