Mkuu wa wilaya
ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na wafanyabiashara wa samaki
katika soko la kuuzia samaki wabichi na wakavu ambalo limevunjwa na kutakiwa kuhamia kwenye soko la
michungwani ambalo limejengwa kwa ubora kwa ajili ya kufanya biashara zote.
Mkuu wa wilaya aliwambia wafanyabiashara hao Pesa ya Serekali na nguvu za
wananchi zimepotea katika kujenga soko haitakuwa vema kama wataendelea kutumia soko
lililovunjwa wakati eneo lililo andaliwa kwa akili yao liko na halitumiki.
Akisisitiza wafanyabiashara
wa soko la samaki wabichi na wakavu kutii na kuondoka eneo hilo na kuhamia soko
la michungwani ambalo limejengwa kwa ubora mzuri kwa ajili ya kufanyia biashara
zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni