Jumatatu, 25 Julai 2016

MWANADAMU KUMBUKA KABLA HUJAFA HAUJAUMBIKA.



Juma Hatibu kijana mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Komesho ambaye alikuwa akifanya kazi katika mashine ya kusaga mahindi iliyopo Mgandini  Kata ya Mabawa Wilayani Tanga alipata ajali ya kuanguka akiwa kazini ndipo alipopata ulemavu mwaka 2001tarehe 30 ya mwezi wa 10.

Kabla ya ulemavu huu kijana Juma alikuwa akufanya kazi zake kama vijana wengine na kuweza kujikimu kimaisha na kusaidia familia .

Juma aliuguu baada ya kuanguka na kutibiwa katika Hospital ya Bombo kisha kupelekwa katika Hospital ya KCMC Moshi ambapo alitibiwa hadi fahamu zake kurudi kwa kiasi .

Baada ya hapo Baba yake mzazi na Juma yaani mzee Hatibu aliomba ruhusa ili warudi nyumbani na kwamaelezo ya Juma waliambiwa ili kijana huyo aweze kurudi katika hali yake ni lazima ahudhurie mazoezi ya mara kwa mara mzazi huyo alikubali kufanya hivyo wakaruhusiwa.

Walirudi nyumbani walipofika Tanga Juma alihudhuria mazoezi katika Hospitali ya Bombo kwa muda wa mwezi mmoja tu na baba yake kumwacha hadi leo kijana huyu ndoto za maisha yake zikizimika taratibu.

Akizungumza kwa uchungu mkubwa Juma amesema kwa sasa hana msaada wa baba wala mtu yoyote wa familia na alipoona hali inakuwa ngumu alimshauri baba yake atafute mke atakaye msaidi na baba yake alikubali na kumuahidi kumsaidia katika huduma za kulisha familia hiyo na hafanyi kama alivyoahidi.

Juma  alipata mke bi Hawa  Amiri na kupata msaada kutoka kwa marafiki na wakafungua biashara ya genge ambalo alikuwa mke akienda kufungasha bidhaa ndogondogo wakabahatika kupata mtoto mmoja wa kiume na kwasababu baba yake Juma alikataa kuwapa msaada kama alivyo ahidi walijikimu kupitia genge lao.

Faida ni ndogo anayopata Juma na mkewe lakini pamoja na maisha magumu wanayoishi chuki zimeibuka kwa mama wa Juma ambaye ni mama wa kufikia na kusababisha mke wa Juma kushindwa kuvumilia na kuondoka.

Juma anahitaji msaada wakati wote na mkewe ndiyo aliyekuwa msaada mkubwa kwake, kwasasa mkewe hayupo hali yake ni ngumu sana.

Juma anaomba jamii  na watanzania wote kumsaidia apate mahali atakapoweza kuishi na mkewe na kufanya biashara zake.

MWANADAMU KUMBUKA KABLA HUJAFA HAUJAUMBIKA LEO KWA JUMA KESHO KWA MWINGINE WANADAMU TUSAIDIANE.

MUNGU AKUBARIKI KWA MSAADA WAKO KWA ATAKAEGUSWA.

Namba ya Juma ni 0716-927126 au 0785-681000.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni