Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akihutubia Maafisa, Askari na
watumishi wote wa Jeshi hilo wakati akifungua zoezi la uchangiaji damu
salama ambalo lilishirikisha vituo vyote vya Zimamoto mikoani, ufunguzi huo
ulifanyika katika viwanjwa vya Zimamoto na uokoaji mkoa wa Ilala.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akichangia
damu katika zoezi lililofanyika viwanja vya kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa
wa Ilala zoezi lililoshirikisha vituo vyote vya Zimamoto mkoa wa Dar es Salaam.
Maafisa,
Askari na watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka katika vituo
vya Zimamoto Makao Makuu, Chuo, Ilala, Kinondoni, Temeke na uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere wakimsikiliza Kamishna Jenerali wakati akihutubia katika ufunguzi wa zoezi la uchangiaji Damu salama
lililofanyika katika viwanja vya Zimamoto mkoa wa Ilala.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amewaongoza viongozi waandamizi,
maafisa, askari na watumishi wote wa jeshi hilo katika zoezi la uchangiaji damu
salama ili kutimiza dhima ya kuokoa maisha ya watu wanaopoteza maisha kwa ajali
za moto, ajali za barabarani, vifo vya mama wajawazito wanaopoteza damu nyingi
wakati wa kujifungua na magonjwa mbalimbali kama vile ukimwi, malaria, anaemia
na kansa.
Zoezi hili limefanyika katika
viwanja vya kituo cha jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa ilala kwa
kushirikiana na taasisi ya mpango wa damu salama ulio chini ya wizara ya afya
maendeleo ya jamii, jinsia watoto na wazee.