Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Omari Kombo akiapokea maelekezo ya jinsi ya kutengeneza sabuni kutoka kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mtimbwani
Katibu –Tume
ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Mkinga Thomas Mnkande akizungumza na wananchi
pamoja na wanafunzi katika mahadhimisho ya Juma la Elimu iliyofanyika Kijijini na Shule ya Mtimbwani
Kaimu Afisa
Elimu Sekondari Wilaya ya Mkinga Rose Kinyamagoha akitoa taarifa fupi ya Elimu
kwa mwaka wa 2016-2017 Wilaya ya Mkinga
Mgeni rasmi
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Omari Kombo akiongea na Wazazi na Wanafunzi
wa Shule na Kijiji cha Mtimbwani katika sherehe ya Juma la Elimu iliyofanyika
Kiwilaya katika Shule ya Mtimbani.
TANGA:
WILAYA ya Mkingi ni kati ya wilaya 8 za mkoa wa Tanga,katika Halmashauri ya Wilaya ya hiyo inajumla ya shule za Sekondari 15 za Serikali na shule za msingi 80 na shule 1 ya msingi ya binafsi.
TANGA:
WILAYA ya Mkingi ni kati ya wilaya 8 za mkoa wa Tanga,katika Halmashauri ya Wilaya ya hiyo inajumla ya shule za Sekondari 15 za Serikali na shule za msingi 80 na shule 1 ya msingi ya binafsi.
Katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
kwa mwaka 2016 Wilaya ya Mkinga haikufanya vizuri kulinganisha na miaka
iliyopita ambayo ufaulu wake ulikuwa 44.2% hivyo Wilaya imejiwekea mikakati
itakayo saidia kuinua ufaulu katika Wilaya hiyo.
Katika Juma la elimu Wilayani Mkinga iliyohazimishwa
katika kijiji cha Mtimbwani viongozi wa Wilaya hiyo wamenia mamoja kukabiliana
na changamoto inayoikabili sekta ya elimu kwa kushirikisha wazazi pamoja na
jamii kwa ujumla ili kutatua changamoto za elimu kwani kwasasa Mtu yoyote anayesababisha
mtoto kukosa elimu ni Muuaji.
Akizungumza katika maadhimisho hayo kaimu Mkurugenzi Halmashauri
ya Mkinga Omary Kombo amesema changamoto kubwa inayoikabili sekta ya elimu wilayani
humo ni utoro, mimba, na ushirikiano hafifu wa wazazi na walimu, ushirikiano wa
Serikalia za vijiji na kata hali inayosababisha ugumu katika kudhibiti watoto
watoro.
Kombo amesema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa
miundombinu ya shule hususani ni vyumba vya madarasa 741 na matundu ya vyoo
1340 pamoja na nyumba za walimu 669 hivyo ameiomba jamii kushirikiana na Halmashauri
kuhakikisha wanapunguza changamoto zanazokabili sekta hii.
Pia Kombo amesema kwasasa Halmashauri imejipanga
kukabiliana na changamoto ya Mimba kwa wanafunzi kwa kujenga hostel katika
shule mbili za Sekondari ili kufwatilia taaluma mara kwa mara na kuwafanya
wanafunzi kuepuka vishawishi.
Kwa upande wake Katibu wa tume ya utumishi wa walimu
Wilaya ya Mkinga Thomas Mnkande amesema kwa sasa wamejipanga kukabiliana na
upungufu wa walimu kwani kwa sasa wana upungufu mkubwa walimu wa Sayansi kwa
shule za Sekondari na wilaya imepokea walimu 12 lakini bado uhaba upo.
Mnkande ameiomba Serikali ikumbuke Wilaya ya Mkinga Kwa kuwapatia
Walimu wa Sayansi ili kuhakikisha elimu bora inamfikia kila mtoto kwani Elimu
bora ni haki ya mtoto.
Naye
mmoja wa wazazi Fortnata Chande kutoka kijiji cha Kasera ameishukuru
Serikali ya awamu ya tano kwa sera yake ya elimu bure kwani
imewapunguzia mzigo wananchi wake na pia usawa katika maisha tumeuona.
Chande
amesema kwa sasa wazazi inatupasa kuwa karibu na walimu pia kujitahidi
kuwanunulia watoto wetu mavazi ya shule, viatu ,madaftari na begi ya
kubebea daftari na kuhakikisha watoto wanakwenda shuleni kwani serikali
inatoa elimu bora kwa watoto hadi ukomo wa uwezo wao.
MWISHO
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni