Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na
usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na
tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.
Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.
“Nimeshtushwa
kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka
zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi
kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani
wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni