TANGA:
JESHI la
Polisi Mkoa wa Tanga yaendesha Operesheni ya kudhibiti makosa usalama
barabarani upande wa waendesha pikipiki iliyoanza tarehe 22/aprili mwaka huu inayoendelea
mpaka sasa na kufanikiwa kukamata pikipiki zenye makosa mbalimbali.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi
mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba amesema idadi ya pikipiki zilizokamatwa ni
225 kwa makosa yafuatayo:
Pikipiki zenye ubovu zilikuwa 50, Pikipiki ambazo
hazikuwa na helment ni 58 , Pikipiki moja ilizidisha abiria(kutunga mshikaki)
Pikipiki 74 madereva wake hawakuwa na D/licence.
Kamanda Wakulyamba amesema zipo hatua mbalimbali ambazo
zimechukuliwa ikiwa ni kufikishwa mahakamani na mpaka sasa wamiliki 19 wamefikishwa
Mahakamani na wengine 15 kulipa fain na
zoezi likiwa bado linaendelea kwa mkoa mzima.
Pia kamanda Wakulyamba amesema Pikipiki 33 zimekamatwa
kwa makosa yanayohusiana na Mamlaka ya Mapato (TRA) na mpaka sasa pikipiki 184
bado zinashikiliwa na polisi kwa Wilaya ya Tanga.
Jeshi Polisi mkoa linaendeleza zoezi hili, kwa kila
Wilaya na Operesheni hii itahusisha vyombo vyote vya usafiri kwani kwasasa ajali
za barabarani zimekua kero kwa watembeaji kwa miguu na watumiaji wa vyombo vya
moto.
“Wito umetolewa na kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga
Benedict Wakulyamba kwa kuwataka watumiaji wa barabara kufuata sheria za
usalama barabarani na kutii sheria bila shuruti”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni