TANGA.
Viongozi waandaaji wa Tanga City Marathon inayotarajiwa kuanza kesho tarehe 15 majira saa 12 asubuhi wamesema mpaka majira ya saa 12 jioni ya leo hii tayari wamepokea washiriki kutoka mikoa mbalimbali hali inaonyesha hadi kufikia majira ya saa nne usiku wakusitisha usajili wanariadha 600 watakuwa wamesajiriwa.
Akizungumza na
Tanga one blog mratibu wa Tanga City Marathon Juma Mwijasho amesema wamepokea
washiriki na wanaendelea kupokea mpaka ifikapo saa nne usiku leo hii itakuwa
mwisho wa kujisajili.
Viongozi waandaaji
wa Tanga City Marathon wamewaomba wananchi na wakazi wa Jiji la Tanga
kujitokeza kuwashangilia ili kuwatia moyo
wanariatha watakao shiriki katika mashindano hayo ambayo ni ya kwanza kwa mkoa
wa Tanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni