Jumatano, 12 Aprili 2017

JESHI LA POLISI MKOA TANGA LIMESEMA LITAWACHUKULIA HATUA WAZAZI WATAKAO WAACHIA WATOTO KUZURURA MITAANI KIPINDI CHA SIKUKUU YA PASAKA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba  akitoa taarifa za matukio kwa Waandishi wa habari mkoa wa Tanga.
Waandishi wa habari mkoa wa Tanga wakimsikiliza kamanda wa polisi akipiga marufuku kupigwa kwa mziki katika kumbi mbalimbali kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Pasaka.

TANGA 
JESHI la Polis Mkoani Tanga limetoa onyo kali kwa wazazi watakao waacha watoto kuzagaa ovyo mitaani wakati wa sikuku za pasaka na kwamba litachukuwa hatua za kisheria kwa mzazi atakae bainika kufanya kosa hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo na kamanda wa polisi Mkoani hapa Benedict Wakulyamba  wakati wa mkutano wake na waandish wa habari ,ambapo alizungumzia hali ya usalama kwa mkoa mzima pamoja na jeshi la polisi namna lilivyojipanga kuzua matukio ya kihalifu hasa kwa nyakati za sikukuu.

Kamanda Wakulyamba amesema Jeshi hilo litawachukulia hatua kali wazazi wenye tabia ya kutelekeza watoto hasa nyakati za sikukuu pamoja na kupiga marfuku disco toto huku akifafanua kwamba Mkoa wa Tanga hauna maeneo maalumu kwa michezo ya watoto.

,,Marufuku kwa kumbi za starehe kuweka disco toto Tanga kwa sababu hakuna ukumbi maalumu kwa ajili ya watoto hivyo atakae kaidi  amri hii atachukulia hatua, ninawataka wazazi waambatane na watoto wao hasa nyakati za sikuku sio kuwaacha watoto wakizagaa ovyo mitaani na sehemu za starehe nasema tutawakamata,, alifafanua kamanda Wakulyamba.

Awali kamanda Wakulyamba akitoa taarifa yake ya mwenendo wa matukio ya kiuharifu  kwa mwezi machi ambapo kesi 1687 zilifunguliwa kwa mwaka huu wa 2017 ambapo sawa na pungufu ya kesi 1756 ambazo zilifunguliwa kipindi kama hicho  sawa na pungufu ya asimili 4.1 na kusema kwamba kutokana na takwimu hizo hali ya mkoa ni shwari.

Aidha jeshi la polisi pia limewaonya watu watakao bainika kujihusisha na milipuko ya aina yoyote na akatoa  ufafanuzi wa sheria ya milipuko na kwamba atakaebainika atachukuliwa hatua za kisheria na kwamba adhabu yake ni fain ya shilingi milioni tano au kifungo kisichopungue miaka 3


                                                         Mwisho.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni