Waandishi wa
habari wakiwa ofisi ya Takukuru mkoa wa Tanga wakimsikiliza Kaimu Mkuu wa
Takukuru Mkoa Sadiki Nombo ofisini kwake. (ambaye hayupo pichani)
TANGA
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga wamefanikiwa
kuokoa fedha za Serikali sh Milioni 83,873,902 ambazo zilikuwa zipotee lakini zimeweza
kurudishwa serikalini.
Hayo yemesemwa na kaimu mkuu wa Takukuru mkoa
wa Tanga Sadiki Nombo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
ambapo amesema fedha hizo zimeokolewa katika sekta mbalimbali ikiwepo Sekta ya
Afya, Elimu Ardhi ,Madini na serikali kuu .
“Nombo amesema fedha hizo zimepatikana kutokana na
malipo hewa ya mishahara kwa watu wasiostahili, madurufu ya misitu yaliyovunwa
kinyume cha utaratibu pamoja na posho zilizolipwa kimakosa katika idara na
taasisi mbalimbali za Umma.”
Pia kaimu mkuu
wa Takukuru mkoa wa Tanga amewaeleza waandishi wa habari kuwa elimu wanayoitoa
kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari imeweza kusaidia kupata taarifa
kwa wananchi ambapo jumla ya taarifa ya 222
ya vitendo vya rushwa wakizilalamikia
idara mbalimbali za Serikali.
Aidha Taasisi
hiyo imefanikiwa kuendesha kesi 16 ambapo kati ya
kesi hizo 8 zilizofunguliwa katika kipindi cha Julai 2016 hadi Machi 2017 huku
kesi 16 zilizoendeshwa mahakamani,na
kesi 5 zilitolewa hukumu ambao watuhumiwa hao hawakukutwa na hatia.
Nombo amesema
katika jukumu la kuelimisha na kuhamasisha umma katika mapambano dhidi ya rushwa
amewaomba wananchi na wakazi wa mkoa wa Tanga kuendeleza ushirikiano na kutoa
taarifa za vitendo vya rushwa katika jamii na hatimaye kuvitokomeza kabisa
kwani Tanzania bila Rushwa inawezekana.
Kaimu mkuu
wa Takukuru mkoa wa Tanga amewataka wananchi wote wenye Taarifa ya vitendo vya
rushwa ndani ya Jiji la Tanga kufika katika ofisi zao zilizopo Jingo la Bandari
ghorofa no 5 chumba no 512 au ofisi zao zilizopo wilaya zote mkoani Tanga pia amesema
unaweza kupiga simu ya bure no 113 au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa
kupiga * 113 #.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni