Viongozi na wasimamizi
wa Tanga City Marathon wakiwa katika ukumbi wa Mkwabi super market wakati wa
kikao pamoja na waandishi wa habari.
TANGA.
Zaidi ya
Wanariadha 300 wamejitokeza kujiandikisha katika mashindano ya Tanga City Marathon
yanayotarajiwa kufanyika April 15 Jijini Tanga.
Akizungumza
na waandishi wa habari Juma Mwijasho amesema bado wanapokea washiriki mpaka siku
ya ijumaa tareha kumi na nne saa tano usiku hivyo wananchi waendelee kujitokeza
kwani mashindano haya ni ya kwanza kwa mkoa huu.
Pia
amesema
hadi sasa wameandikisha wanariadha kutoka mkoa mbalimbali ya nchi hii
ikiwemo Arusha, Dare s salaam, Manyara, Mbeya na wengine kutoka mtwara.
Kwa upande
wake Meneja wa Mkwabi Kaukap Hussen amesema anawashukuru wadau mbalimbali
waliofanikisha maandalizi ya mashindano hayo na kwamba kwa sasa yamekamilika.
“Amesema Mashindano
hayo yaliyodhaminiwa na wadau mbalimbali yataanzia katika jengo la Mkwabi super
market yatakuwa ni ya kilometa 21, 10 na
kilometa 5 ambapo yataishia katika viwanja vya mkwawani” Amesema Kaukap.
Akizungumzia
swala zawadi Kaukap amesema kwa mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21
atakabidhiwa shilingi milioni moja huku mshindi wa pili atapata shilingi laki
saba,mshindi wa 3 atapata laki 5 na wengine watapata medali.
Naye
mkurugenzi wa matukio na uandaaji Nassoro Makau amesema kwamba burudani
mbalimbali zitakuwepo katika viwanja vya mkwakwani huku akiwataka wananchi
kujitokeza kwa wingi kuwa tia moyo.
“ Nitowe
wito kwa nanchi wa Tanga kujitokeza katika maeneo ambapo wanariadha hao
watapita ili kuwashangilia naamini italeta hamasa na kuwatia nguvu wanamichezo
wetu” alibainisha Makau
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni