WAZIRI wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame
Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa
Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13
ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu
kuanzia tarehe 10.04.2017.
Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo
kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada
ya uteuzi wa awali kufika ukomo.
Aidha, sambamba na uteuzi huo Prof. Mbarawa amewateua
Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania kuanzia
tarehe 10.04.2017 kama ifuatavyo:-
1.Eng. John Bura – Mkandarasi kupitia Bodi ya Usajili
wa Makandarasi (CRB)
2.Arch. Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi.
3.Prof. Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam.
4.Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali.
5.Eng. Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni