Shamba la Miti la Halmashauri ya Jiji la Tanga lililopo Mleni kata ya
Mzizima lililopandwa miti mwaka 2011
ambalo ni theruthi ya shamba lenye ukubwa wa Hekta 65
Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebose akipanda mti katika maadhimisho
ya siku ya Mazingira katika shamba la Miti la Mleni kwa kushirikiana na wanafunzi
pamoja wananchi wa kata ya Mzizima.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa akipanda
mti katika shamba la Miti la Halmashauri ya Jiji hilo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mleni wakishiriki katika upandaji miti
katika shamba la Halmashauri ya Jiji la Tanga mtaa wa mleni kata Mzizima.Afisa Maliasili Jiji la Tanga Aneni Nyirenda akitoa taarifa ya shamba la miti la Mleni kwa Meya wa Jiji la Tanga Mustaph Selebose ambaye hayupo kwenye picha.
Mwenyekiti wa mtaa wa mleni Shaban Ibrahim akizungumza na viongozi wa Jiji kuwakumbuka wananchi wa Mleni na kuwapatia miti ili nao waweze kupanda kutunza mazingira.
TANGA.
Halmashauri ya Jiji la Tanga ofisi ya Maliasili imejipanga kuwekeza katika kilimo cha miti katika shamba la Mleni lililopo kata ya Mzizima na kuwataka wananchi kutenga nusu hekta kwajili ya upandaji wa miti itakayo saidia familia kwa kizazi kijacho.
Hayo yamesemwa na Meya wa Jiji wa Tanga Mustapha Selebose katika wa siku ya Mazingira ambayo ilifanyika kiwilaya kata ya Mzizima mtaa wa Mleni ambapo miche ya Miti 2500 ilipandwa.
Selebose amewashukuru wakazi wa Mleni kwa ulinzi wa Miti kwani hakuna historia ya uchomaji wa shamba la miti hiyo pia amewataka wananchi wazitumie mvua zinazonyesha kipindi hiki kwa kupanda miti ili kutunza mazingira kwani ni uwekezaji na utajiri wa baadaye.
Pia amewataka kutenga maeneo kwenye mashamba yao kwajili ya kupanda miti itakayo wasaidia watoto na wajukuu zao baadaye.
Selebose amemtaka Afisa Maliasili wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha usalama wa shamba la Jiji ambalo ni hekta 65 zilizopimwa ili wananchi wasilivamie na kulilima ili kuongeze uwekezaji kwa kupanda miti.
Kwa upande wake Kaimu Mkugenzi wa Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa amewataka wananchi kuwa na mazoea ya utunzaji wa mazingira na kupanda miti itakayowapa faida baadaye.
Gwakisa amesema huu ni uwekezaji mkubwa ambao Halmashauri ya Jiji la Tanga limejipanga kuelekeza nguvu kuhakikisha shamba linalimwa na kupandwa miti.
Naye Afisa Maliasili Jiji la Tanga Aneni Nyirenda amesema katika shamba la Mleni lililoanza kupandwa mwaka wa 2011 na kwa sasa miti iliyopo inaumri wa miaka minne na katika shamba kuna mizinga ya nyuki isiyopungua kumi na Tano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni