Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela akipanda mche wa mkorosho katika mafunzo kwa
wakulima wa korosho kutoka Wilaya sita za Mkoa wa Tanga.
Wakulima wa korosho kutoka Wilaya ya mbalimbali za mkoa wa Tanga wakiwa katika
mafunzo ya Kilimo cha korosho yanayoendeshwa na Bodi ya Korosho Tanzania na
kufanyika katika Chuo cha Kilimo Mati Mlingano
Mkanyageni Wilayani MuhezaTANGA:
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, amewapiga marufwakulima kutumia madalali katika uuzaji wa mazao yao na kuagiza bodi ya Korosho Tanzania tawi la Tanga, kuhakiksha lengo la Serikali la kuzalisha tani laki tano za korosho ifikapo mwaka 2025.
Akifungua
mafunzo ya siku tatu kwa wakulima wa zao la korosho katika Chuo Cha Kilimo Mati Mlingano Wilayani Muheza
Mkoani Tanga na kuwashirikisha maofisa
ugani pamoja na wataalamu wa kilimo cha korosho , Shigela amesema Serikali
imeiagiza bodi ya korosho kugawa miche ya korosho kwa kila kaya.
Shigela
amewataka wananchi na wakazi wa mkoa wa
Tanga kujikita katika uchumi kwa kilimo
kwa kuitumia ardhi yao kwa kulima korosho kwani soko lake linakuwa kila siku
ndani na nje ya nchi.
“Kama
bodi ya korosho Tanga itatekeleza agizo
la Serikali kuhakikisha inagawa miche kila kaya miaka mitano ijayo kila mkulima
atakimbilia kilimo cha korosho” alisema Shighela.
Shigela
amesema Tanga tuna ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo cha korosho hivyo hatuwezi kushindwa
na wenzetu ambao hawana ardhi kama ya kwetu,
hivyo tuhakikishe tunaitumia vizuri ili ilete manufaa kwa jamii na kuhakikisha kilimo cha korosho hapa mkoani kinakuwa juu na
kila mmoja ananufaika” alisema
Mkuu
wa mkoa wa Tanga amewataka wakulima kufuata miongozo ya wataalamu walioko kila
Wilaya ili kilimo chao kiwe na tija na
kusema kuwa soko lipo hivyo kuongeza bidii kwenye kilimo.
Kwa
upande wake, Kaimu Meneja Bodi ya Korosho Tawi la Tanga, Frenk Mfutakamba, amesema
wamefikia asilimia 80 ya usambazaji wa miche ya mkorosho kwa kugawa bure kwa
wakulima.
Bodi
ya Korosho itahakikisha inagawa miche mipya kila kaya ili kuweza kufikia
malengo ya Serikali kuzalisha tani laki tano ifikapo mwaka 2025.
Naye
mkulima wa kilimo cha korosho Mkanyageni Wilayani Muheza, Zaidu Ramadhani
ameitaka bodi ya Korosho Tanzania kuwasogezea karibu maduka ya pembejeo za
kilimo.
Ramadhani
amesema huwa wanasafiri kwenda Dar es Salaam kufuata pembejeo kwa gharama kubwa
hivyo kutaka kuwasogezea ikiwa na pamoja na kupunguza gharama za ununuaji wa
bidhaa za kilimo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni