Alhamisi, 6 Aprili 2017

TANGA CEMENT YAKABIDHI HUNDI YA MILIONI 14 KWA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA.



Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda Cha Saruji cha Simba Cement Tanga , Renhardt Swart akitoa  maelekezo kuhusu utendaji kazi wa Kiwanda kwa Wanachama wa Jukwaa la Wahariri (TEF) walipotembelea kiwandani hapo.
Wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda Cha Saruji cha Simba Cement Tanga mara tu walipowasili kiwandani hapo.
Makamu mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF)Deudas Balile akipokea Hundi ya shilingi Milioni 14 kutoka Kiwanda cha Tanga Cement.

 Wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF)wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kiwanda cha Simba Cement Tanga.

Wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) wakijivinjari katika maeneo ya mbalimbali ya uzalishaji katika kiwanda cha Cement cha Simba kilichopo mkoani Tanga.

TANGA

UONGOZI wa kiwanda Cha Saruji cha Simba Cement Tanga,kimeiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya umeme inayo kikumba kiwanda hicho nakufanya washindwe kufika malengo ya uchumi wa viwanda.


 Akizungumza na wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)waliofika kutembelea  kiwanda cha Saruji kujionea shughuli ambazo zinafanywa, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart, alisema pamoja na changamoto zilizopo zipo faida ambazo wananchi wa maeneo ya jirani wanazipata ikiwa ni Elimu ,Afya, Ajira pamoja na utunzanji wa Mazingira.

Renhardt Swart amesema kiwanda cha Saruji cha Simba kimekuwa msaada kwa jamii kwa kusaidia ujenzi wa majengo mifuko ya saruji na pamoja na vyoo kwa shule ambazo zimekuwa zikihitaji msaada na madawati kwa shule za jirani.

Akikabidhi  hundi ya shilingi milioni 14 kwa Makamu mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Deudas Balile, Swart amesema pesa hizo zinaweza kuwasaidia katika majukumu  yao mbalimbali ukiwemo mkutano mkuu ambao unaanza tarehe 6 machi  huko Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deudas Balile, amesema kiwanda cha saruji cha Simba nikiwanda ambacho kimejipanga uzalishaji wa Saruji  iliyo bora na amefurahishwa na mipango thabiti ya Uongozi wa Simba Cement .

Pia Balile amesema fedha walizosaidiwa na Simba Cement Tanga zitawasaidia katika shughuli za maendeleo ya Jukwaa hilo na kuwataka wawekezaji kuunga mkono shughuli zinazofanywa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).



                                    MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni