Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe
(watano kushoto) akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Nchemba (katikati) wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka
hiyo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa NIDA katika hotuba yake
fupi kwa Waziri Mwigulu, alisema kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho
kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wananchi hao
wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta (TEHAMA) wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mohamed Khamis (wapili kushoto) alipokuwa akielezea jinsi wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri Mwigulu alitembelea Kituo hicho cha Usajili na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu
ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Mwigulu aliwaambia waandishi wa
habari kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia
mwezi Desemba mwaka huu, ambao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,
Andrew Massawe.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni