Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Novemba, 2016 amemteua
aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Bw. Diwani Athuman
kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.Uteuzi wa Bw. Diwani Athuman unaanza mara
moja.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika
taasisi tano za Serikali kama ifuatavyo.
Kwanza, Rais Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA)
Uteuzi huu umeanza tarehe 16
Novemba, 2016.
Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Bw.
Sylvester M. Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA).
Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba,
2016
Tatu, Rais Magufuli amemteua Prof. Patrick Makungu kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo
(TEMDO).
Uteuzi huu umeanza tarehe 16
Novemba, 2016.
Nne, Rais Magufuli amemteua Bw. Martin Madekwe kuwa mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.
Uteuzi huu umeanza tarehe 17
Novemba, 2016.
Tano, Rais Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa
Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya
Kitropiki Tanzania (TPRI)
Uteuzi huu umeanza tarehe 17
Novemba, 2016.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU
Dar es Salaam
18 Novemba, 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni