JESHI la Polisi Mkoani Mwanza limewafukuza kazi askari watatu kwa
tuhuma za kukiuka maadili ya kazi ikiwemo kujihusisha na vitendo vya utovu wa
nidhamu pamoja na upokeaji wa rushwa.
Akizungumza na askari hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,
Ahmed Msangi amesema hatua imechukuliwa ili iwe fundisho kwa askari wengine
wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi hiyo.
Amesema askari mmoja kati ya hao amekutwa akiwa amelewa na
kulala lindoni, huku wengine wawili wakituhumiwa kujipatia pesa kwa njia ya
udanganyifu.
Kamanda Msanga amesema ukiukwaji wa maadili ni chanzo cha
ongezeko la uhalifu hivyo hatamvumilia askari yoyote atakaye kwenda kinyume kwa
kufanya hivyo kunalichafulia hadhi jeshi la polisi kwa sababu ya makosa ya
askari wachache.
Kamanda Msingi ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha askari
kufuata weledi wa kazi zao na kusema askari wanaotumia vyeo vyao kwa ajili ya
kujipatia pesa kutoka kwa wananchi atawatumbua kabla kasi hiyo ya utumbuaji
haijamfikia kwa kushindwa kuwasimamia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni