Siku chache baada ya kuripotiwa taarifa za kukamatwa kwa
mwanaume mmoja kutoka Malawi ambaye inadaiwa alikuwa akiwanajisi watoto wadogo
wanaotajwa kufika 100 kwa maelezo kwamba anawasafisha na kufanya tambiko la
kimila, Hatimaye amehukumiwa kwenda jela miaka miwili.
Hukumu hiyo imeonesha kutotenda haki kwa watoto hao kutokana
na uchache wa miaka aliyofungwa mwanaume huyo. Tayari mashirika ya kutetea haki
za binadamu na asasi za kupambana na maambukizi ya virusi vya HIV nchini Malawi
zimekosoa hukumu hiyo
Michael Chipeta, wakili na mwanaharakati wa kutetea haki za
binadamu nchini humo amekosoa hukumu hiyo na kusema kuwa kulikuwa na mapungufu
mengi katika mchakato mzima wa kesi na hukumu dhidi ya mwathirika huyo wa
virusi vya HIV, anayejulikana kama Eric Aniva mwenye umri wa miaka 45.
Eric Aniva alikiri kwamba amefanya ngono na wasichana wadogo
kwa kulipwa fedha ambazo ni dola nne mpaka saba za Marekani kwa kuondoa
usichana wa (kubikiri) kila mtoto mmoja, kwa imani kuwa ubikira ni mkosi na
kwamba kitendo hicho kinawasafisha watoto hao pamoja na jamii hiyo.
Malawi ni katika nchi zenye maambukizi makubwa ya virusi vya
Ukimwi duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni