NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiwa ameongozana na timu ya Serikali
yenye wataalamu na wanausalama wameendesha operesheni kali ya kusaka viroba
feki na pombe nyingine haramu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na
kufanikiwa kukama shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo
hayo.
Katika operesheni hiyo, pia wamefanikiwa kukibaini kiwanda bubu kinachotengeneza kinywaji aina ya konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza Jijini Dar es Salaam.
Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia
‘spirit’ ambayo inachanganywa na ‘gongo’; spirit, gongo, chupa tupu na
zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa.
Kwa hatua hiyo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili
ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye
anatafutwa na polisi mpaka sasa kwa tuhuma za kuendesha shughuli hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni