SERIKALI ipo kwenye mpango wa kuanza utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya afya katika kila kata nchi mzima ili kumaliza changamoto ya upungufu huo uliopo kwa sasa katika maeneo mengi.
Rai hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala na mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo wakati wa ziara yake wilayani Pangani.
Alisema mpango huo unatarajiwa kuanza utekelezaji wake kuanzia mwaka ujao wa fedha kwa kila Halimashauri kujengewa kituo kimoja cha afya katika ngazi yakata .
Pia alisema kupitia mpango huo serikali itaweza kwa kiasi fulani kufikia lengo la lake iliyojiwekea la kila kata kuwa na kituo cha afya ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa licha ya utekelezaji wa Sera ya afya kutiliwa mkazo katika maeneo mengi hapa nchini bado mpaka sasa Tanzania mzima inavituo vya afya 440 pekee.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah alisema kuwa wilaya hiyo inakata 14 lakini ina kituo cha afya kimoja hali inayosababisha changamoto ya utoaji wa huduma.
“Wilaya
yetu maeneo kata nyingine zimetenganishwa na mto Pangani hivyo kutoka na hali
hiyo tumelazimika kujenga kituo cha afya katika kata za ngambo ili tuweze
kuwahudumia wananchi wote" alisema Dc huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni