Hakimu Mkazi Mwandamizi Juma Hassan ametoa hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Hassan amesema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo upande wa mashitaka walipeleka mashahidi watano akiwemo daktari kutoka Hospitali ya Amana Dar es Salaam.
Hakimu Hassan amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo upande huo wa mashitaka umeweza kuthibitisha mashitaka bila kuacha shaka yoyote.
Akisoma baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo Hakimu Hassan alisema mshtakiwa ni baba yake mdogo na mtoto huyo, ambapo walikuwa wanalala chumba kimoja.
"Mshitakiwa ni baba yake mdogo na huyu mtoto, alitueleza kuwa alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo mara nyingi huku akitishiwa kuuawa pindi atakaposema kwa mtu yeyote," alisema.
Pia alisema kuwa baba yake na mtoto alikuwa anafanya kazi za usiku na mama yake, vivyo hivyo na kwamba mshtakiwa mara nyingi alikuwa anakaa na huyo mtoto ndipo alianza kumfanyia vitendo hivyo akiwa darasa la pili.
Hakimu alisema kutokana na ushahidi wa Daktari pamoja na mtoto umeweza kuthibitisha mashitaka hayo kwani mtoto hawezi kutoa ushahidi wa uongo.
Kabla ya kutolewa adhabu, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga aliomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo kama hivyo.
Aidha, mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea ni kwa nini asipewe adhabu kali, aliomba kupunguziwa adhabu akidai kwamba yeye hajatenda kosa hilo kwani amesingiziwa. Hata hivyo, Mahakama ilitupilia mbali maombi hayo na mshitakiwa kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Inadaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Septemba na Desemba mwaka jana eneo la Kiwalani Migombani wilayani Ilala kwamba alimlawiti mtoto wa miaka tisa kinyume na sheria za nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni