WAJUMBE wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi Baraza la
Uwakilishi la Zanzibar wametembelea
bandari ya Tanga eneo la upakuaji wa shehena ya mizigo na kutazama fulsa za ujio
wa Mradi wa Bomba la Mafuta Mkoani Tanga.
Wajumbe hao 14 wakiongozwa na
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamza Hassan Juma walitembelea eneo itakapojengwa
bandari mpya ya Mwambani Tanga wamesema fulsa hizi zitaongeza ajira kwa vijana
wakiwemo Wanzanzibar waishio Tanga.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Hassan alisema
Serikali ya Zanzibar imejipanga kuimarisha bandari zake ikiwemo ya Wete na
Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni maandalizi ya ujio wa Bomba la Mafuta.
Akizungumzia kilio
cha wafanyabiashara na wasafiri wa Pemba na Tanga kwa kutumia usafiri wa
baharini, Hassan alisema kero hiyo Serikali inaitambua na jitihada za kuwa na
meli ya uhakika inafanywa.
Alisema baadhi ya wafanyabiashara wa Pemba ambao walikuwa
wakichukua bidhaa Tanga wamekatisha na baadhi yao mitaji kufa kutokana na
kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika wa baharini.
Awali akizungumza na wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi,
Kaimu Meneja wa Badari Tanga, Henry Arika, alisema mchakato wa mradi wa bomba
la mafuta unaenda kwa kasi na kuwataka wawekezaji kutoka Zanzibar kuja
kuwekeza.
Arika alisema Tanga ziko fursa nyingi za uwekezaji na yako maeneo mengi hivyo kupitia ujio wa
mradi wa Bomba la mafuta amewataka wawekezaji wa ndani kuchangamkia fulsa
zilizopo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni