Kamishna wa Operesheni ya Mafunzo Jeshi la Polisi Nsato Marijani Mssanzya akiteremka kwenye gari kuelekea katika maeneo yaliyokuwa maficho ya majambazi waliokuwa wakifanya uharifu katika wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.
Kamishna wa Operesheni ya Mafunzo Jeshi la Polisi Nsota Marijani Mssanzya akiwaeleza waandishi wa habari na kuwaonyesha silaha zilizo kamatwa katika msako wa waharifu waliofanya matukio katika mkoa wa Tanga kushoto kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba na wa pembeni ni Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Tanga Hamediuc Tesha.
Hili ndiyo eneo ambalo majambazi walichimbia silaha walizo kuwa wakifanyia uhalifu ambazo kwa sasa zimesha kamatwa na ziko mikononi mwa Jeshi.
Askali Polisi wakiwa kazini wakati wa ziara ya Kamishna wa Opereseni ya Mafunzo Jeshi la Polisi Mkoani Tanga.
Kamishina wa operesheni ya Mafunzo Jeshi la Polisi akibadilishana mawazo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba akizungumza kitu na Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Tanga Hamediuc Tesha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba akiwatoa hofu wakazi wa Tarafa ya Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga na kuwataka waendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa.
WATU wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi, wameuawawa na Polisi mkoani Tanga, wakiwa njiani kwenda kuonesha silaha wanazotumia katika matukio mbalimbali ya uhalifu mjini hapa.
Sanjari na kuuwawa kwa majambazi hayo pia jeshi hilo limefanikiwa kupata silaha 9 zikiwa na risasi 425 wanazotumia kwenye matukio ya uhalifu wa katika chuo kikuu cha Secomu na kuua watu wasiokuwa na hatia.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika eneo la kijiji
cha Kibandai kilichopo kata ya Kwemashai, Mlalo Lushoto mkoani hapa,
Kamishina wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Msanzya alisema watu hao
wameuawawa wakiwa katika harakati za kupelekwa porini
kuoneshwa silaha hizo.
kamishina wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Msanzya aliwataja waliouwawa kuwa ni Murdick Ally Abdi maarufu kwa
Jina la Osama mkazi wa Mbagala Dar es salaam (24) na Sultan Khalid
Khatwabi (24) mkazi wa Kiembesamaki Unguja ambao Walipokamatwa walikiri
kuhusika na matukio mbalimbali.
Watu hao wakiwa njiani Kamishina Msanzya alisema walitamka
maneno ya Allah Akbar ndipo kulipolia risasi ambayo ilimjeruhi askari
aliyekuwa mbele akitangulia na wenzake pamoja na majambazi hayo.
"wale majambazi waliposema Allah Akbar walimkurupusha
jambazi mwingine ambaye alipiga risasi iliyomjeruhi polisi wetu na wale
majambazi walikimbia porini na askari wakajibu kwa kupiga risasi na
kuwauwa, " alisema Kamishina Msanzya.
Hata hivyo, katika msako mkali katika eneo hilo ambapo
Oktoba 19 wakafanikiwa kupata SMG saba zikiwa na makasha ya kuhifadhia
risasi 'Magazine', 16 na risasi 425, bunduki aina ya Rifle yenye risasi
7 na Short gun ikiwa na risasi 25.
Vitu vingine vilivyokutwa kwa majambazi hayo ni redio za
upepo 'redio call' zipatazo saba, bendera nne zenye maandishi ya lugha
ya kiarabu na mavazi ya kuziba nyuso.
Kamishina huyo aliyekuwa ameongoza na Kamishina Lebaratus
Sabas pamoja na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba,
alisema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha Wanawadhibiti watu wote
waliopanga kuvuruga amani ya nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni