Lipumba alifanya kazi hiyo akitekeleza agizo la Rais John
Magufuli la kufanya usafi Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi. Msemaji wa CUF,
Abdul Kambaya alisema haoni kama ni jambo la ajabu kwa Lipumba kufanya usafi
wakati akilindwa.
“Sioni mantiki ya swali hilo,
suala la kulindwa Lipumba siyo wa kwanza,”
alisema
Mapema jana, polisi mjini Tanga ilizuia mkutano uliopangwa
kuhudhuriwa na Maalim Seif ambao ulipaswa kuwajadili madiwani 12 waliopigana
wiki iliyopita katika ofisi za chama hicho wilayani humo, baada ya kugawanyika
kuhusu uamuzi wa wenzao waliohudhuria baraza la madiwani wa jiji hilo Oktoba
12.
Taarifa ya jeshi hilo ilidai kuzuiwa kwa mkutano huo ni
kutokana na tisho la uvunjifu wa amani na kuwapo kwa makundi mawili
yanayozozana. Mkutano huo ulipangwa kufanyika katika Hoteli ya Mkonge mjini
hapa.
Pia, taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga,
Idd Abdallah ilisema ukumbi ambao mkutano huo ungefanyika ni mdogo kutokana na
wingi wa wanachama.
“Ukumbi uliopangwa
kufanyika kwa mkutano huo ni mdogo na ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mkutano wa
chama hicho ngazi ya wilaya ulivunjika kutokana na vurugu,” alisema
Akizungumzia sakata hilo, Mwenyekiti wa CUF wa wilaya hiyo,
Rashid Jumbe alisema hata kama jeshi hilo limezuia mkutano huo, lengo la chama
kuwajadili madiwani hao liko palepale.
Alisema kamati ya utendaji imependekeza madiwani saba kati
ya 12 wafukuzwe uanachama kutokana na kukiuka msimamo wa chama na watano
watabaki chini ya uchunguzi.
“Katika fagio hili mbunge (Mussa
Mbaruku) pia yumo kwani naye alishiriki kikamilifu pamoja na naibu meya
(Mohamed Aniu), kwa sasa tunafanya utaratibu na jeshi la polisi kutekeleza
masharti na vigezo wanavyotaka ili kuufanya mkutano huo tena,” alisema.
Profesa Lipumba akipigiwa saluti na askari wa Jeshi
la Polisi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni