Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waliohudhulia hafra ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa hosteli
za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam .
HABARI KAMILI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli ameagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu kutumia Sheria zilizopo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni kwa
wahitimu walionufaika na mikopo.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo
leo jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa
hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unajengwa na Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) kwa gharama ya shilingi bilioni 10.
Amesema kuwa Serikali inadai
takribani shilingi trilioni 2.6 kwa wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya
juu.
“Serikali inawadai wahitimu
walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu takribani shilingi trillion 2.6 ambazo
wanatakiwa kuzirudisha ili ziweze kutolewa kama mikopo kwa wanafunzi wapya na
waliopo vyuoni” alifafanua Dkt Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli ameitaka
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kusimamia ipasavyo
suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi kwa kuzingatia vigezo vilivyopo kwani
lengo la mikopo hiyo inawalenga watoto maskini.
Alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya
malalamiko ya kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
inafanya zoezi la ugawaji wa mikopo hiyo kwa upendeleo hivyo kuzitaka uongozi
wa Wizara kushughulikia suala hilo.
Mbali na hayo Rais Magufuli
amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimia mikopo hilo kwa malengo mazuri
katika kujinufaisha na masuala ya Elimu.
Naye Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa mradi
wa ujenzi wa hosteli hizo utasaidia kuwahudumia wanafunzi 3,840 ambapo
unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi Desemba 2016.
Katika hatua hiyo Prof. Ndalichako
alisema kuwa wanafunzi waliodahuiliwa kwa mwaka huu wapo 58,000 hivyo suala la
wanafunzi 66,000 kukosa mikopo hiyo ni upotoshaji unaofanya na baadhi wa watu.
Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za
wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wenye majengo 20 kila jengo gorofa
nne zenye vyumba 12 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni