Ndege mbili mpya za Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400 zinatarajia kuanza kazi wakazi wa
mikoa ya Mwanza, Arusha na Zanzibar watakuwa wa kwanza kupata ofa.
Ofisa Habari wa shirika hilo, Lilian
Fungamtama amesema safari mpya za ndege hizo ikiwamo ya Dar es
Salaam - Mwanza, nauli iliyopangwa ni Sh160,000.
Amesema safari za Dar es Salaam
- Arusha nauli yake itakuwa Sh180,00 na Zanzibar - Dar es Salaam ni Sh85,000.
“Ofa hii imetolewa na ATCL kwa
safari mpya za ndege hizo,” alisema Fungamtama.
Amesema hakutakuwa na safari ya moja
kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, lakini itakuwapo ya kutoka Dar
es Salaam -Arusha hadi Zanzibar.
“Ndege ya kutoka Dar es Salaam
kwenda Arusha ndiyo itakayokwenda kuchukua abiria Zanzibar haitatokea Dar es
Salaam moja kwa moja,” alisema.
Akifafanua kuhusu nauli hizo,
Fungamtama alisema nauli ya kutoka Dar kwenda Kigoma itakuwa katika
madaraja mawili ambayo ilikuwapo tangu awali.
Amesema bado ndege hizo hazijaanza safari katika mikoa yote
hadi hapo watakapotangaza.
Akizungumzia safari za nje ya nchi,
alisema itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam - Hahaya hadi Comorro ambayo nauli
yake ni Sh543,950 kwenda na Sh926,650 kwa kwenda na kurudi.
“Lengo letu ni kutoa huduma
nzuri itakayomridhisha kila mteja,” alisema Fungamtama.
Mbona sioni safari ya kutoka dar kwenda tanga?
JibuFutaJamani mbona dar to tanga hamna au sisi pesa hatuna jaman
JibuFutaMbona nauli Ni Bei kubwa kuliko mliyotutangazia?
JibuFutaNaomba nauli ya dar to Zanzibar
JibuFutaNaomba nauli ya dar to Zanzibar
JibuFutaDar to tanga ?
JibuFuta