Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27
Oktoba, 2016 amemteua Bw. Samwel Peter Kamanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Bw. Samwel Peter Kamanga ameteuliwa kushika wadhifa huo kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2016.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Samwel Peter Kamanga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni