Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuutaarifu
umma kuwa, kwa mujibu wa vifungu vya 8 na 16 vya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa
Sura ya 147, wazalishaji wote wa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa na
wazalishaji wa malighafi ya kutengenezea spiriti wanatakiwa kusajiliwa na
kupewa leseni na Kamishna Mkuu wa TRA kabla ya kuanza uzalishaji.
Bidhaa
zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa zimeainishwa katika jedwali la nne la Sheria
husika. Baadhi ya bidhaa hizo ni kama Bia, Sigara, Spiriti, Mvinyo
na
Vinywaji baridi.
Masharti ya Leseni
1.
Maombi
yote yatumwe kwa Kamishna Mkuu kwa kutumia fomu ya maombi ya leseni
inayopatikana katika ofisi za TRA au tovuti: www.tra.go.tz
1.
Maombi
tofauti yafanywe kama ifuatavyo:
1.
Kwa kila
kiwanda ambacho kitatumika kuzalisha bidhaa. Leseni itatumika kwa kiwanda
kilichopewa leseni pekee
2.
Kwa kila
aina ya bidhaa itakayozalishwa na leseni itatumika kuzalisha bidhaa husika
pekee.
1.
Mmiliki wa
leseni hataruhusiwa kuhamisha umiliki wa leseni husika, kubadili kiwanda au
kuzalisha bidhaa tofauti katika kiwanda kilichopewa leseni bila kufanya maombi
na kuruhusiwa na Kamishna Mkuu.
1.
Baada ya
kupewa leseni, mzalishaji anatakiwa kumjulisha Kamishna Mkuu juu ya tarehe ya
kuanza uzalishaji ndani ya siku 21 tangu uzalishaji huo kuanza.
1.
Pindi
bidhaa yoyote inapoamuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge kuanza kutozwa Ushuru
wa Bidhaa, mzalishaji wake anapaswa kumjulisha Kamishna Mkuu na kuomba leseni
ya uzalishaji ndani ya siku 21 baada ya bidhaa husika kuanza kutozwa Ushuru wa
Bidhaa.
1.
Leseni ya
uzalishaji itakwisha muda wake kila tarehe 31 Disemba ya mwaka ambapo mmiliki
atatakiwa kuomba leseni mpya.
1.
Wazalishaji
wa spiriti yenye vionjo na isiyo na vionjo (Denatured and Undenatured Spirit)
pia wanatakiwa kuomba leseni za uzalishaji kwa Kamishna Mkuu.
Uzalishaji wa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa
bila ya leseni ni kosa linalopelekea adhabu ya faini au kifungo au faini na
kifungo ikiwa ni pamoja na kutaifishwa kwa mitambo na bidhaa zote zilizohusika
katika utendaji wa kosa hili.
Wazalishaji wote wanaaswa kumiliki leseni halali
katika wakati wote wa uzalishaji na TRA kwa kushirikiana na wadau wengine
wataendesha ukaguzi endelevu kuhakiki matakwa haya ya sheria.
Waombaji wanatakiwa kufanya maombi katika ofisi
yoyote ya TRA ambako viwanda husika vinapatikana ili kuepuka adhabu kali
zinazotokana na ukiukwaji wa matakwa haya ya sheria.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu
Dar es Salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni