Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akifungua kikao cha pili cha bodi ya barabara katika ukumbi wa ofisi ya mkoa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella wa pili kutoka kulia akifwatilia makabrasha ya kikao cha bodi ya barabara kushoto kwake ni Katibu Kawala Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said , kulia kwake ni mbunge wa jimbo la mlalo Rashidi Shangazi na Mbunge wa Muheza Adadi Rajabu
Mbunge wa Pangani Jumaa Aweso akizungumza neno na mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdalah.
Mbunge wa Korogwe vijijini Stevin Ngonyani (Profesa Maji
Marefu) Mbunge wa korogwe Mjini Mery Chatanda wakijadiliana na Mbunge wa
Pangani Jumaa Aweso katika mkutano wa Bodi ya Barabara katika ukumbi wa ofisi
ya mkuu wa mkoa Tanga.
HABARI
MKUU
wa
Mkoa wa Tanga Martin Shigella amewaomba wabunge wa Mkoa wa Tanga kuishinikiza
serikali kutilia mkazo utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango
cha lami unaounganisha wilaya Mkoa pamoja na mikoa ya jirani.
Katika kampeni za urais zilizofanyika mwaka Jana Rais John Magufuli aliahidi kutekeleza ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Saadani pamoja na Handeni kupitia Kilindi hadi Singida kwa kiwango cha lami.
Akifungua kikao cha pili cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Tanga kwa mwaka wa fedha 2015/16 kilichofanyika hapo Jana alisema kuwa kufunguka kwa barabara hizo kutaweza kuinua fursa za kiuchumi za Mkoa huo.
Aliwaomba wabunge wa Mkoa huo kuhakikisha wanaikumbusha serikali kuhusu kutekeleza ahadi hiyo kwa haraka ili wananchi waweze kufaidika na fursa zilizopo za kibiashara na kiuchumi.
kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kilindi Omar Kigua alisema kufunguliwa kwa barabara hizo kutaziwezesha wilaya za Handeni na Kilindi kufungua fursa za kiuchumi hususani maeneo ya Kilimo na mifugo.
"Uchumi wa Mkoa utafunguka endapo barabara zitafunguka tuone namna ya kuweka nguvu ya pamoja ili tuweze kufungua uchumi wa Tanga, hivyo tuzipe nguvu ili ziweze kupitia kwa mwaka mzima" alisema Kigua.
Hata hivyo Mbunge wa Pangani Jumaa Aweso alisema kuwa uchumi wa sekta ya utalii katika wilaya ha Pangani unaporomoka kutoka na uchakavu wa miundombinu ya barabarAweso
Tanga Saadani.
"Kutoka na umuhimu wake ndio maana nimekuwa nikipiga kelele bungeni kuhusu serikali kuharakisha ujenzi wa barabara hii,hivyo naamini katika kikao hiki tutakuja na maazimio mazuri " alisema Aweso
Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Steven Ngonyani alisema kuwa watendaji wa TANROADS tuambieni mahali mnapokwama katika kuwasilisha taarifa za ujenzi wa barabara ili tuweze kuwasaidia.
"Kama kuna mahali kuna zuia kupitisha barabara basi tuambieni sisi wabunge tutazifanyia Kazi kwani haiwezekani kwa miaka zaidi ya kumi tunapiga kelele ya ujenzi wa barabara ambazo hautekelezeki" alisema Ngonyani.
Hata hivyo Mbunge wa Jimbo laMuheza Balozi Adadi Rajabu alisema kuwa serikali lazima ione umuhimu wa kutoa kipaumbele katika barabara ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya wilaya husika na Mkoa kwa ujumla.

Nae Meneja wa wakala wa barabara TANROADS Mkoa wa Tanga Alfred Ndumbalo alisema kuwa tayari serikali imeshakamilisha upembezi yakinifu wa barabara ya Handeni ,Kilindi Hadi Singida kwa kiwango cha lami lakini kuna hitilafu katika ujenzi wa madaraja.
Ambapo serikali imemuagiza mhandisi mshauri aweze kufanya tathimini upya wa madaraja yaliyopo katika barabara hiyo ili yaweze kuendana na matumizi ya barabara hiyo.
"Madaraja ya awali yalikuwa ni madogo sana ambayo yangeweza kusombwa hata na Maji hovyo baada ya kuliona hilo tumemuagiza Mhandisi mshauri afanye marekebisho hayo ili aweze kukabidhi Kazi mapema" alisema Ndumbalo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni