MEYA wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi
amefikwa na umauti jana majira ya saa tatu na nusu usiku katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu yake, Dk.
Makongoro Mahanga ambaye alieleza kuwa familia ipo katika taratibu za awali za
msiba huo na kwamba leo watatoa taarifa rasmi na taratibu nyingine.
“Taarifa za kifo cha Dk. Masaburi
ni za kweli ingawa sijaenda hospitali, ninafanya mawasiliano na familia lakini
taarifa kamili kuhusu msiba zitakuwa zikitolewa na msemaji wa familia ambaye
tutamteua usiku huu, na kesho (leo) tutaeleza kiundani,” Alisema Dk. Mahanga jana usiku.
Marehemu pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki (EALA).
Mtandao huu unatoa pole kwa Taifa kwa ujumla kwa msiba huu
wa aliyekuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali akiutumikia umma. Apumzike kwa Amani.
Amina!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni