Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ukamataji wa bidhaa hizo kamanda wa polisi
mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba amesema wanefanikiwa kukamata mifuko ya 214
ya sukari, mifuko ya 138 ya mchele na madumu 132 ya mafuta katika bandari bubu
zilizopo mkoani humu.
Pia jeshi la
polisi limefanikiwa kuwakamata watu 9 wakiwemo wanawake 2
na wanaume 7 kwa kosa la kukutwa na dawa za
kulevya aina ya mirungi, bangi na heroin.
Kamanda wakulyamba
amesema wamefanya oparesheni iliodumu
kwa muda wa siku 7 lilifanikiwa kukamata
bangi kg 300 ,mirungi kg 647 pamoja na heroin gram 39.
Hata hivyo
jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
Samsoni Karanga (36) aliyekuwa akitokea arusha kwenda mbeya akiwa na hati za
kusafiria (Passport) 14 zenye majina tofauti za afrika ya kusini pamoja na hati
14 za homa ya manjano.
Kamanda
amesema mtu huyo alikamatwa katika maeneo ya Mombo wilayani korogwe mtuhumiwa
anashikiliwa na polisi wakati utaratibu wa kisheria ukiendelea ili afikishwe
mahakamani.
Kamanda
Wakulyamba ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano na kutoa taarifa
za watu wanaojihusisha na magendo pia kuwataka wananchi kuacha mara moja kwani
kwa sasa magendo siyo biashara ya kufanya na kuwataka wakazi wa mkoa huu
kufanya biashara za halali.
Kwa upande
wake meneja wa TRA mkoa wa Tanga Swalehe Byarugaba amesema zoezi hili ni
endelevu na wamejipanga kuhakikisha wanazuia bidhaa zinazo ingizwa kwa kukwepa
kodi na hazina ubora na baadhi ya bidhaa hizo zimepita muda wake wa kutumika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni