Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba akiwa na Meneja Forodha wa TRA Mkoa wa Tanga Jumbe Magoti mwenye shati la batiki pamoja na mashuhuda katika doria ya kukamata bidhaa za Magendo
kwenye Bandari bubu ya Kigombe wilayani Muheza Mkoani Tanga, Picha ni wakikagua
madumu ya mafuta yaliyo telekezwa
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba akiwa na OCD wa Pangani wakiefwatilia Jahazi
la MV Yarazaki lililokuwa limebeba mali za magendo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba Meneja Forodha wa TRA Mkoa wa Tanga Jumbe Magoti pamoja
na OCD wa Pangani wakiwa kwenye doria ya kukamata bidhaa za Magendo
kwenye Bandari bubu ya Kigombe wilayani Muheza Mkoani Tanga.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba Meneja Forodha wa TRA Mkoa wa Tanga Jumbe Magoti wakikagua moja ya chombo kinachotumika kuingiza bidhaa za magendo kutoka nchi mbalimbali.
JESHI la polisi mkoa wa Tanga kwa
kushirikiana na T.R.A Uvuvi Doria
alfajiri ya tarehe 19/3/2017 katika doria ya pamoja kwenye bandari bubu ya kigombe kata ya
Kigombe Wilayani Muheza Mkoani hapa wamefanikiwa kukamata Jahazi moja yenye
namba za usajiri Z 1221 MV Yarazaki ambayo Nahodha na Mmiliki hajafanikiwa kikiwa
na Shehena ya bidhaa za Magendo.
Akizitaja
bidhaa ambazo zimekamatwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba
amesema tumekamata (1) Mafuta ya kula aina ya oki dumu 304 za lita 20, kutoka
Indonesia, (2) Sukari Mifuko 64 ya kutoka Blazil (3) Mchele mifuko 10 kutoka
Pakistan.
Mpaka Muda
mwandishi wa Tanga One blog anaingia
mtamboni thamani ya bidhaa hizo hazijafaamika gharama yake.
Kamanda
Wakulyamba ametoa wito kwa wale wote wanaofanya biashara za magendo kuacha mara
moja biashara hizo na kufanyabiashara
kwa mfumo raisi wa kulipa kodi kwa ustawi wa nchi yetu.
Pia kamanda
amesema operesheni hizi ni endelevu katika bandari bubu zote na hata nchi kavu
jeshi la polisi mkoani Tanga halite
mfumbia macho yeyote anaye vunja sheria ya nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni