KIKAO cha
utekelezaji wa uhakiki wa mpaka wa wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara na Kilindi
mkoani Tanga kimefanyika katika ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Tanga na kujumuisha viongozi mbalimbali kutoka katika mikoa yote
miwili.
Katika kikao
hicho ambacho kilihudhuliwa na waziri wa Adhi Nyumba na Makazi William Lukuvi
ambaye aliwaagiza viongozi wa wilaya husika kuwaelimisha wananchi wa maeneo
hayo ili kufanya zoezi hilo la uhakika mipaka kuisha kwa wakati.
Waziri
Lukuvi alisema mipaka huo wa kilindi na kiteto umeshaakikiwa kwa mara mbili bado mgogoro unaendelea kwa
kipindi cha muda mrefu na hii ni mara ya tatu na yamwisho serikali haita rudia
tena kupima mpaka huu.
Lukuvi
alisema serikali haianzishi mpaka mpya ila katika mpaka uliopimwa kipindi cha
nyuma na kuwekewa alama za mapipa ambayo yaliliwa na kutu itawalazimu
kufwatilia na kuweka alama za guzo kama za barabara zisizo haribika
kilahisi.
Hata hivyo Lukuvi
alisema wizara itatoa wapima kutoka nje ya mikoa hiyo miwili ili kujenga imani na wananchi pia
wapima hao watatoa taarifa kwa viongozi na wananchi ili kujua maendeleo
ya zoezi hilo.
Waziri Lukuvi alisema gn 65 ya mwaka 61 ndiyo itakayo
ongoza kwani mipaka hii ilisha pimwa na inaongozwa kwa mujibu wa mamalaka na
mujibu wa kisheriaya nchi.
Waziri Lukuvi
amewahakikishia wananchi wa mikoa miwili Tanga na Manyara kufanya kazi zao kwa
amani na hakuna mwananchi atakaye bughudhiwa na zoezi hili la uhakiki
litakapoanza .
Kwa upande
wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella alisema mkoa wa Tanga umeridhia na
uamuzi uliotolewa na kikao hicho cha viongozi kutoka mikoa yote miwili pamoja
na Waziri mwenye dhamana hivyo kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za
ujenzi wa taifa.
Shigella
alisema wizara imelichukua hili kulifanyia kazi na wananchi watoe ushirikiano
pale wapima watakapo fika mkoani ili mgogoro uweze kuisha na wananchi wa wilaya
ya kilindi na kiteto kuisi kwa amani .
Naye mkuu wa
mkoa wa Manyara Joely Bendela alimshukuru waziri Lukuvi kufanya maagizo ya
waziri mkuu Kassim Majaliwa kwa vitendo ili
kuondoa mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya Kilindi na Kiteto.
Bendera
alisema wananchi wanatakiwa kushiriki kikimilifu katika zoezi ili litakalo
fanywa na wapima kutoka wizara ya Ardhi ilikuonye watanzania kuwa kilindi kuna
amani na kiteto kuna amani hakuna ugomvi.
Pia
amewataka viongozi kuwekea mkazo mpaka huo kwani kwa kufanya hivyo watamaliza
mgogoro wa mpaka huo na amewataka viongozi kutokengeuka katika makubaliano ya
kuhakikisha mgogoro wa mpaka unatokomea kabisa kwani watanzania wote ni ndugu.
mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni