Ijumaa, 17 Machi 2017

WIKI YA MAJI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA YAFUNGULIWA RASMI TANGA.

 Ofisi za mamlaka ya maji na usafi wa mazingira zilizopo mtaa wa swahili jijini Tanga.


Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Tanga Inj Joshua Mgeyekwa kwenye kikao cha pamoja na Waandishi wa Habari katika ukumbi uliopo ofisi za mamlaka ya maji mkoani hapa.

 Inj Mgeyekwa akiwasomea taarifa fupi za utekelezaji na malengo waandishi wa habari waliofika kwenye kikao .


Afisa wa Ankara  Mamlaka ya maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Kuluani Luambo akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kusoma mita kwa waandishi wa habari mkoani Tanga.



Hii ni picha ya mita ya Limaku ambazo zimeanza kufungwa ndani ya Jiji la Tanga Limaku ni Lipia maji kadri unavyo tumia.                                            
 

TANGA



TANZANIA inaadhimisha wiki ya maji kuanzia mwaka wa 1988 na huu ni mwaka wa 29 kwa maadhimisho hayo kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoani Tanga imemepata mafanikio kwa kuongoza miaka mitatu mfururizo kwa kupata cheti cha kuwa mamlaka yenye kutoa huduma bora.

Akizungumza na waandishi wa Habari mkurugenzi mtendaji Inj Joshua  Mgeyekwa amesema mkikati iliyopo ni kuhakikisha wanatoa huduma bora na kuwafanya wadau kuwa makini katika utumiaji wa maji kwani kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Majisafi na majitaka punguza uchafuzi yatumike kwa ufanisi.

Pia amesema mamlaka imejipanda kubadili mita za kieletroniki ambazo mteja atalipia maji kabla hajatumia na mita hizo zimeshaanza kutumika katika nyumba za wanajeshi zilizopo nguvumali pamoja na shule ishirini (20) zimesha fungiwa mita hizo.

Inj Mgeyekwa amesema katika maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza tarehe 16 hadi 22 mamlaka imetoa msamaa kwa wenye madeni sugu kufika ofisi za mamlaka hizo ili kuweza kaorozesha madeni na kuyalipa kwa awamu huku wakirudishiwa maji.

Hata hivyo Inj Mgeyekwa amewataka wakazi wa jiji la tanga wanaokaa katika maeneo ya jirani na mtandao wa majitaka kujiunga na mtandao wa maji taka kwa faida kwani majitaka yanaweza kutumika katika shunghuli mbalimbali za kiuchumi kama kilimo cha umwagiliaji na ufugaji wa samaki.

Mkurugenzi mtendaji amewataka wakazi wa Jiji la Tanga wanaohitaji kubadilishiwa mita kuwekewa mita za Limaku kufika katika ofisi za mamlaka kwajili ya zoezi hilo.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni