Kuelekea maadhimisho
ya siku ya wanawake duniani, hawa ni wanawake wajasiliamali wakiwajibika katika
soko la Msambiazi Wilayani Korogwe.
KATIKA
kuelekea maadhimisho ya
siku ya wanawake duniani, wanawake mkoani Tanga wamejipanga kwa kufanya
makongamano ya kupatiwa elimu ya kushiriki katika kuwekeza kwenye uchumi wa
viwanda.
Hayo yamesemwa na afisa maendeleo ya jamii
Jiji la Tanga Mwantumu Dosi wakati akifungua kongamano maalum yenye lengo la
kuwajenga wanawake katika maswala ya uzalishaji mali na kuweza kupandisha
thamani ya bizaa wanazozizalisha.
Amesema katika kuiunga mkono serikali ili
kuelekea uchumi wa viwanda ni vyema wanawake wakajiandaa kielimu kwa
kuhakikisha watumia vyuo vya veta ili kujikita zaidi katika maswala ya
kuzalisha bidhaa zenye tija na kujua masoko husika ya bidhaa wanazozalisha.
Pia Dosi amewataka wananwake kujiunga katika
vikundi ili jambo ambalo litasaidia kuwajengea uwezo hasa kwa kupata fursa mbalimbali
iliwemo kupata mikopo itakayowawezesha kukuza mitaji yao.
,,Nawaomba
wanawake wenzangu tujiunge kwenye vikundi kwani kwa kufanya hivyo itasaidia
kukopesheka kwani ni rahisi kujidhamini kuliko mtu mmojammoja hivyo tufanye
hivi kwa kujiandaa na uchumi wa viwanda,,anabainisha Dosi.
Wakizungumza
washiriki wa kongamano hilo wamesema changamoto kubwa inayowakabili wanawake
kwa sasa ni mitaji pamoja na mfumo wa maisha ambao umetawaliwa na mfumo dume
jambo ambalo linawarudisha nyuma wanawake wangi katika shughuli zao za
uzalishaji mali.
Fatna
Bendera yeye ni mmoja wa wanawake waliopata fursa ya kushiriki kongamano hilo
ambaye anajishughulisha na uuzaji wa mbogamboga yeye anasema changamoto kubwa
ni mitaji na kwamba wanawake wengi ni wajasiliamali wadogo hivyo wanashindwa
kukidhi mashari ya taasisi zinazotoa mikopo.
Aidha
wamemuomba rais Magufuli kutekeleza ahadi yake ya milioni hamsini kila kijiji
ili waweze kukopa fedha hizo wanaamini kwamba zitawasaidia katika kukuza mitaji
yao.
Wakizungumza
na mwandishi wa Tanga one blog wanawake wa soko la Msambiazi wamesema kila
wanapofanya biashara wanalipa ushuru lakini hawaoni mabadiliko yoyote katika
soko hilo.
Asha
Ramadhani ni mmoja ya wanawake wanaofanya biashara katika soko
la Msambiazi lililopo wilayani Korogwe mkoani Tanga naye ameuomba
uongozi wa soko hilo kuwasaidia kwani wanafanya biashara wakiwa juani na pia
wateja hawaji kwa wingi kwani hata ukaaji wao katika soka hilo sio mzuri.
Naye Shabani
Karimu mkazi wa Manundu Korogwe amesema soko la alhamisi la Msambiazi ni kubwa
na linavutia hata yeye anatoka mjini kuja kufanya manunuzi ya wiki nzima katika
soko hili kwa bei nafuu na vitu vizuri.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni