Alhamisi, 30 Machi 2017

SERIKALI HAITAONGEZA MUDA WA MAKADIRIO YA AWALI YA KODI KWA WAFANYABIASHARA.


Wakazi wa Jiji la Tanga na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika ofisi za Mamlaka ya Mapato  Mkoa wa Tanga (TRA) wakisubiri kufanyiwa makadirio ya awali ya kodi kwa wafanyabiashara na uhakiki wa Tina namba  Zoezi ambalo linatarajia kukoma tarehe 31 ya mwezi 3 tatu kwa mwaka wa 2017.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Tanga Swalehe Biyalugaba akizungumza na mwandishi wa habari wa  Tanga one Blog ambaye hayupo kwenye picha ofisini kwake na kusisitiza wananchi kujitokeza kwajili ya kuhakiki tini na kufanyiwa makadilio ya awali ya kodi za biashara.



Wafanyabiashara  na Wakazi wa Jiji la Tanga na viunga vyake wakiwa kwenye foleni  katika ofisi za Mamlaka ya Mapato  Mkoa wa Tanga (TRA) wakisubiri kufanyiwa makadirio ya awali kodi kwa wafanyabiashara na uhakiki wa Tina namba, Zoezi ambalo litakoma tarehe 31 ya mwezi huu wa tatu mwaka wa 2017. 

TANGA
MAMLAKA ya Mapato mkoa wa Tanga (TRA) Wamewataka wakazi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kuweza kufanya makadirio ya awali ya malipo ya kodi na kuhakiki Tini Namba zao , zoezi ambalo limeanza tangu Machi moja mwaka huu wa 2017.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Tanga Swalehe Biyalugaba amesema msongamano uliopo kwa sasa unatokana na wafanyabiashara  kuchelewa kuhakiki Tini ambayo ni zoezi la kitaifa linalofanyika nchi nzima na kuisha machi 31 kwa mwaka huu.

Wakazi wa Jiji la Tanga na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Tanga(TRA) na kuitaka serikali kuongeza muda kwani kwasasa ofisi ya hiyo wateja ni wengi na muda umekwisha.

Pia wameiomba serikali kuweka tawi jingi ndani ya Jiji hili la Tanga ili kuwapatia wateja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) huduma kwa wakati na kupunguza msongamano na adha wanayokutana nayo.

Naye Husseni Mwangonji amewataka wananchi na wateja wezake kutii pale wanaposikia matangazo mbalimbali ili kuepuka msongamano huu unaowafanya wapoteze muda mrefu kusubiri huduma kwani dakika za mwisho kwa kawaida kunakuwa na msongamano mkubwa na kuwachosha watumishi wa mamlaka ya Mapato.

Hata hivyo amemuomba meneja wa mamlaka ya Mapato Tanga kuongeza watumishi katika vitengo husika ili kuongeza nguvu kwa muda mchache uliobaki.




 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni