Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba na afisa wa TRA Enos Leonad amefanikiwa
kukamata pombe kali ya konyagi zilizo
kwenye vifungashio vya plastiki (viroba)vyenye thamani ya zaidi ya sh ml 86.
Afisa wa TRA
Enos Leonad akiwa na Kamanda wa Polisi wakifanya uhakiki na uthamini wa uhalali
katika swala zima la ulipaji kodi kwa bidhaa.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba amewataka wananchi kushirikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama kuwafichua wanaoendelea kuuza pombe zenye vifungashio
vya plastiki (viroba)
TANGA
JESHI la polisi mkoa wa Tanga kwa
kushirikiana na TRA mkoa wa Tanga imefanikiwa kukamata shehena ya pombe kali
aina ya Konyagi ikiwa kwenye vifungashio vya Plastiki (Viroba)kwenye godauni
ilioko mtaa wa Sentro.
Kamanda Wakulyamba amesema lengo la Serikali sio kuwafilisi wafanyabiasha ila
wanatakiwa kufwata sheria kwani viromba vimeshapigwa marufuku na waziri mkuu
Kassimu Majaliwa kuanzia machi 1 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni