BAADA ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na Wenyeviti wa
Serikali za mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia mihuri
kwa wenyekiti wa serikali za mitaa.
Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi
kutoka serikali za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba
Chawene amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuri kwa
Wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka hapo baadae itakapojadiliwa tena.
''Hakukuwa na dhamira yeyote ya
kupunguza mamlaka ya heshima yenu Wenyeviti, lakini kama mihuri inaweza
kupunguza heshima yenu nimeona kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili
tene upya swala hili" amesema
Sanjari na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa kulikuwa
na sababu za msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri kutokana na
matumizi mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na kupelekea
kuigawa ardhi bila utaratibu maalumu.
Hata hivyo Katibu wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam Mariam
Machicha ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi kulifanyioa
kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni