TAASISI
ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR inatarajia kuanzisha
chuo kikuu cha afya na tiba ili kuweza kukabiliana na upungufu wa
wataalamu wa utafiti wa magonjwa ya binadamu hapa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurungenzi wa Kituo cha utafiti cha Amani Dkt
Willium Kisinza wakati akitoa taarifa ya kituo hicho kwa Waziri wa Afya
,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Ummi Mwalimu wakati ya ziara yake
katika kituo hicho.
Alisema
kuwa chuo hicho kinatarajia kuanza udahili wa wanafunzi wake mapema
mwakani kwa kushirikina na Chuo cha Kumbukumbu ya Sebastiani Kolowa
kilichopo wilayani Lushoto.
Dkt
Kisinza alisema kuwa kuanzishwa kwa chuo hicho kutaweza kusaidia
kuongeza raslimali watu katika kuzalisha watafiti ambao wataweza
kutumika kufanya utafiti nchini na nje ya nchi .
“Tunawatafiti
waliobeba katika ngazi za hadi PHD hivyo tukaona ni wakati mwafaka
kuanzisha chuo ili nguvu kazi iliyokuwepo tuweze kuitumia kufundisha
wataalamu wengine Zaidi ambao watakuja kuwatumikia wananchi wa nchi
hii”alisema Mkurungenzi huo.
Aidha
Kwa upande wake Waziri Ummi Mwalimu alisema kuwa licha ya serikali
kujitahidi kuzalisha wataalamu lakini bado hatujaweza kufikia kiwango
kile kinachohitajika na umoja wa mataifaWHO.
Alisema
kuwa kwa sasa serikali inajitahidi kujenga vyumba vya upasuaji katika
kila wilaya hivyo ni vema chuo hicho kikaweza kuona umuhimu wa kuanzisha
kozi ya maswala ya maabara pamoja na utafiti wa magonjwa ya binadamu.
“Tunanunua
vifaa tiba vingi lakini changamoto kubwa iliyokuwepo ni uhaba wa
wataalamu wa kutumia vifaa hivyo hususani sekta ya maabara na waatalamu
wa dawa za usingizi hivyo kuanzishwa kwa chuo hicho kutasaidia kupunguza
uhaba uliopo “alisisitiza Waziri Mwalimu.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu alisema kuwa
wananchi wa Amani walikuwa wanaliona eneo hilo la ekari 227.8kama
limetelekezwa huku likiwa na miundombinu ya kuanzishwa chuo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni