MKUU wa wilaya ya Lushoto January Lugangika ametoa siku 14 kwa
wanafunzi waliotakiwa kuripoti shule kwa ajili ya kuanza masomo ya kidato cha
kwanza wawe wamefanya hivyo kabla ya hatua za kisheria dhidi yao
hazijachukuliwa.
Agizo hilo alitoa Mara baada ya
kufanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya ujenzi wa maabara katika shule ya
sekondari ya Bernard Membe iliyopo katika kata ya Kwakanga wilayani humo.
Alisema kuwa shule hiyo ilipangiwa
wanafunzi 90 lakini toka shule zilipofunguliwa mpaka sasa ni wanafunzi
Tisa pekee ndio waliweza kuripotia kwa ajili ya kuanza masomo shuleni hapo huku
81 wakiwa hawajaripoti.
" Lugangika amemwagiza mwenyekiti
wa kijiji kwa kushirikiana na mgambo wawakamateni wazazi ambao watoto wao
hajaripoti shule wahojini na wakishindwa kuripoti shule basi nileteeni taarifa
tuwapeleka mahakamani wazazi wote ambao watoto wao wamefaulu na wameshindwa
kiwapeleka shule".
Aidha katika hatua nyingine aliagiza
baada ya wiki mbili kupita wazazi wote ambao watashindwa kutoa ushirikiano
ikiwemo kupeleka watoto wao shule basi wapelekwe mahabusi.
Hata hivyo Mkuu wa shule hiyo ya
Sekondari Boniface Winifred's wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya shule hiyo
alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu hususani wa
masomo ya sayansi.
Alisema kuwa hali hiyo inachangia
kwa kiasi kubwa uwepo wa utoro kwa wanafunzi na wale wapya kuvunjika moyo wa kuja
kupata elimu katika shule hiyo.
"Changamoto nyingine
muindombinu iliyopo sio rafiki kwa mwanafunzi wala walimu kuweza kufanikisha
lengo la utoaji wa elimu kwani kuna mpaka uhaba wa madarasa pamoja na vitabu
vya kiada " alisema Mwalimu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni