Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustaph Selebose akiwa na Mbunge wa Tanga Mussa Mbaruku akizungumza na wasafirishaji wa mabasi yaendayo Mombasa baada ya kutokea kutoelewana kati ya Askari wa Jiji na wamiliki wa Mabasi hayo
HABARI
ASKARI wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na
kumlazimu Mbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasi na Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingilwa na wafanyabiashara hao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.
Magari
hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu
na Assad Hotel ambapo kulikuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasa nchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata
moja ya gari linaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kutoa faini.
na Assad Hotel ambapo kulikuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasa nchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata
moja ya gari linaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kutoa faini.
Baada ya
kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge Mussa Mbaruku ambaye yupo mkoani Tanga
mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoani Dodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua
kufika eneo la tukio na
kuwachukua askari hao kwa gari
lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisi zao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini
Tanga.
Akizungumza
na wasafirishaji hao,Mbunge Mbaruku aliwataka kuwa watulivu kwani suala hilo linajadilika na
huenda likapatiwa ufumbuzi kutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo
vinatarajiwa kuketi hivi
karibuni mjini hapa.
karibuni mjini hapa.
Aidha
Mbunge Mbaruku alishtushwa na kitendo cha askari hao
kuchukua ushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyume na utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
kuchukua ushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyume na utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Hata hivyo
askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambaye alisema wao wanafanya
kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo na wanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa
ya kukamata gari zote ambazo
zinatakiwa kupaki kwenye stendi
kuu ya Kange.
Alisema
kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo
na atakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi elfu 50,000 jambo lililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine za kielektroniki.
na atakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi elfu 50,000 jambo lililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine za kielektroniki.
Aidha pia
mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za
Tanga Mombasa Mohammed Nassor alisema swala lilowashtua zaidi ni kutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jambo ambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.

Akizungumzia
sakata hilo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mustapha Selebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs na
hawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashine hizo.
Alisema
wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari na kulipeleka depo ya
Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu za
kutozwa faini kwa mfumo wa mashine.
kutozwa faini kwa mfumo wa mashine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni