Mwandishi wa habari Amina Omari akimpa pole mtoto Said
Muhamed Said ambaye amepona katika ajali ya boti la MV Burudani ikitoka Tanga
kwenda Pemba.
Baba mkubwa wa Said Muhamed Said akimtambua mtoto wake
mmoja aliyepata ajali ya Boti ya Mv
Burudani iliyopata ajali usiku saa saba
Mtoto Cheupe akiwa amelazwa katika hospitali ya bombo
kwa matibabu baada ya kunusulika katika ajali ya MV Burudani.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo Dkt. Godlack
Mbwilu akieleza waandishi wa habari walivyo pokea majeruhi na maiti katika
Hospitali hiyo kutokana na ajali ya Boti MV Burudan.
JESHI
la
polisi mkoa wa
Tanga limefanikiwa kwaokoa abiria wa boti ya 27 wa Boti ya Mv Burudani
waliopata ajali usiku wa kuamkia leo wakiwa njiani kutoka Tanga kuelekea Pemba
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi
mkoani Tanga Benadict Wakulyamba amesema wamepokea majeruhi 27 na maiti kumi na
mbili (12) hadi saa nane mchana lakini jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la
uokoaji faya na bandari pamoja na
wananchi bado wako kwenye eneo la tukio kaangalia kama wataweza kuokowa wengine
waliobaki wakiwa hai au maiti.
Naye kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo Dkt.
Godlack Mbwilu Amethibitisha kupokea majeruhi 25 wanaoendelea na matibabu katika
hospitali ya bombo na maiti 12 ikiwa ni
watoto 6 na watu wazima ni 6 na mpaka saa nane mchana bado hawajatambuliwa.
kaimu mganga mfawidhi amewataka wananchi kujitokeza kutambua maiti zao
katika hospitali ya Bombo.
NA KWA TAARIFA ZAIDI ENDELEA KUTEMBELEA
BLOG YA SAUTI YETU WANATANGA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni