RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na
Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia
Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam JANA
Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na
Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali na kampuni
washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).
Pamoja na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na Wataalam wa
pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya makubaliano
rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha
wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi
kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka
Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania.