HABARI
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto
wamejidhatiti kutatua changamoto zinazoikumba sekta za afya nchini ili
kutengeneza Taifa lenye wananchi imara kwa maendeleo ya jamii na uchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano
mkuu wa kutathimini nakurekebisha Sera ya Afya uliofanyika Jijini Dar es
Salaam.
“Katika mkutano huu tumeadhimia kuongeza bajeti ya
dawa nchini kutoka milioni 31 mpaka kufikia milioni 231 ambazo zitachangia
kuondoa uhaba ambao umejitogeza hivi karibuni”Alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa katika mkutano huo
wanatarajia kupata njia za kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba Sekta ya
afya nchini.
Kwa Mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa sekta ya Afya
inaupungufu wa watumishi kwa asilimia 49 hivyo kunauhitaji mkubwa wa watumishi
katika sekta hiyo ambapo watahitajika ili kuimarisha huduma bora.
Amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kupata kinga
juu ya magonjwa ya sioambukizwa ikiwemo kisukari, Magonjwa ya moyo na shinikizo
la damu ambapo watazindua kampeni ya mazoezi ya viungo Desema 17 mwaka huu
Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa wamejipanga
kuhakikisha zahanati zote za serikali zinatumia mashine za Kieletroniki katika
kukusanya mapato ya sekta za afya ili kuboresha Huduma.
Wakati huo huo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipokea msaada wa magari ya kubebea
wagonjwa (Ambulance) 10 kwa ajili ya hospitali za Tanzania kutoka ubalozi
wa Qatar nchini.
Akipokea magari hayo Waziri Ummy amesema kuwa magari
hayo yatasambazwa katika hospitali za rufaa ilikusaidia kupunguza idadi ya vifo
vya wagonjwa wanaocheleweshwa kutokana na kukosa usafiri wakuwahishwa
kwenye hospitali nyingine.
Aidha Waziri ummy alibainisha hospitali zitakazopata
magari hayo ni Mombotanga, Benjamini Mkapa Mbeya, Taasisi ya Jakaya kikwete
Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Dodoma na Ruvuma, hospitali ya
Kigamboni na NzegaTabora.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni