Jumatatu, 19 Desemba 2016

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI AMEAGIZA ZICHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA KWA MKANDARASI ALIEHUSIKA UPOTEVU WA FEDHA ZA SERIKALI


NAIBU waziri wa  Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ameagizwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wakandarasi waliohusika na upotevu wa fedha zaidi ya sh Bil2.7 za miradi ya kujenga mabwawa matatu ya maji katika wilaya ya Handeni ambayo yameshindwa kutoa maji.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akiongea na wananchi wa kata ya Mkata mara baada ya kutembelea bwawa mojawapo lililopo katika eneo hilo ambalo toka lilipokamilika mwaka jana limeshindwa kutoa maji kwa kiwango kinachotakiwa.

Alisema kuwa katika wilaya hiyo taarifa zinaonyesha tayari kiasi cha sh Bil 2.7 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa ya Manga ,Mkata pamoja na Kwenduga ambayo fedha zimekwenda lakini hakuna matokeo bora .

"Hatuwezi kuvumilia upotevu mkubwa wa fedha huku wananchi wetu wakiendelea kupata shida ya maji,hivyo nikuagize mkurungenzi niletee majina ya wataalamu wote waliohusika katika usimamizi na ujenzi wa miradi hiyo ili waweze kuchukuliwa hatua"alisema Naibu Waziri huyo.

Alisema kuwa serikali ya awamu hii imejikita kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 kila mwananchi mahali alipo awe anapata huduma ya maji safi na salama bila kulazimika kutembea umbali mrefu.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri alisitisha ujenzi wa bwawa la malezi mpaka hapo wataalamu kutoka wizarani watakavyo upitia upya mradi huo na kujiridhisha kuwa unaweza kuleta tija kwa kutoa maji yatakayoweza kumaliza uhaba uliopo.

"Nasitisha matumizi ya fedha Mil 500 ambazo tayari zimekuja katika Halimashauri kwa ajili ya utekelezaji wa hatua za awali kwani inaonyesha kabisa eneo hili halina uhakika wa maji huku tayari fedha imekwisha idhinishwa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwen Gondwe alisema ili kudhibiti upotevu wa fedha za miradi wilayani hapo amewaagiza wataalamu wa maji kuipitia upya maandiko ya miradi yote ambayo haijatekelezwa ili kujiridhisha kama inalingana na thamani halisi za fedha zilizotengwa.

Alisema kuwa kama miradi mingine ya maji ingeweza kutekelezwa vizuri kwa kuzingatia viwango vya ubora ikiwemo mradi mkubwa wa HTM basi wilaya hiyo isingekuwa na tatizo la uhaba wa maji kabisa.

"Tunaishukuru serikali kupitia wizara kwa kutupatia kiasi cha Bil 2 kwa ajili ya ukarabati wa muindombinu ya maji katika mradi wa HTM ambao naamini ukarabati wake utakapokamilika utaweza kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi"alisema Mkuu wa wilaya hiyo.

Hata hivyo Mhandisi wa mradi wa maju unaounganisha wilaya za korogwe na Handeni Shemzingwa Bilal alisema kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati huo haziwezi kutosheleza mahitaji.

"baada ya kuufanyia upembuzi yakinifu mradi huo mwaka 2014 ili kukarabati mradi huo kulihitajika kiasi cha Bil 120 ambazo zitahusisha ujenzi wa muindombinu ya mabomba,kuongeza eneo la bwawa pamoja na kukarabati njia za maji"alisema Bilal.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni