Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Tanga Nassoro Sisiwaya
akitoa taarifa ya usalama barabarani kwa mkoa ya mwaka 2015/ 2016
katika kiwanja cha Tangamano katika maadhimisho ya wiki ya usalama
barabarani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba akizungumza na
wananchi watumiaji wa barabara katika wiki ya usalama barabarani mkoani
Tanga katika kiwanja Tangamano.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Tobias Mlapwa akizungumza na wananchi pamoja na
viongozi wa mbalimbali na watumiaji wa nyombo vyamoto katika wiki ya
usalama barabarani Mkoani Tanga iliyofanyika viwanja vya Tngamano mkoani
Tanga.
Viongozi mbalimbali Wadau wa usalama barabarani Mkoa wa Tanga akiwemo
mkuu wa wilaya ya Tanga Tobias Mlapwa Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa
Tanga na Viongozi wa kamati ya usalama barabarani.
Askari wa kikosi cha zima moto na ukoaji mkoani Tanga akimpa maelezo
mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Tanga katika shughuli za wiki ya usalama
barabarani mkoa wa Tanga.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa wamesimama kwa
ukakamavu wakimsikiliza mtoa elimu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa
akitoa taarifa ya jinsi walivyojipanga kupambana na madereva
wanaokwenda mwendo kasi na wanaotumia vilevi kwa mgeni rasmi katika
maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani mkoa wa Tanga iliyo kamilishwa
hii leo katika kiwanja cha Tangamano kilichopo Jijini Tanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni